SOMALIA-UN-USALAMA

Waziri wa Somalia ni miongoni mwa waliouawa katika shambulizi la Alshabab

Mwanajeshi wa Somalia akiokoa majeruhi katika jengo lililoshambuliwa mjini Mogadishu
Mwanajeshi wa Somalia akiokoa majeruhi katika jengo lililoshambuliwa mjini Mogadishu REUTERS/Feisal Omar

Shambulizi la Alshabab dhidi ya jengo la serikali mjini Mogadishu limegharimu maisha ya watu 11 akiwemo naibu waziri wa kazi,serikali nchini somalia imethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo lililothibitishwa kutekelezwa na wanamgambo wa Al shabab linaashiria kuwa kundi hilo lenye msimamao mkali bado linauwezo wa kuyumbisha usalama katikati mwa taifa la Somalia licha ya miaka kadhaa ya misaada mbalimbali ya kijeshi kwa serikali ya Mogadishu.

Seneta Ilyas Ali Hassan amethibitisha kwamba naibu waziri wa kazi Saqar Ibrahim Abdalla,ameuawa katika shmabulizi hilo.

Ripoti zinadai Milipuko miwili iliyotekelezwa katika lango kuu la kuingia ofisi hizo ndio ilianza kusikika kabla ya washambuliaji kuvamia majengo ya wizara ya kazi.

Wanawake watatu ni miongoni mwa waliouawa katika shambulizi hilo ambapo majeruhi ni 15.

Kwa mujibu wa polisi wapiganaji wanne wa Alshabab walivamia ofisi hizo za serikali kabla ya kusikika kelele za makabiliano na wafanyakazi waliokuwemo katika majengo hayo.