MALI-MAUAJI-USALAMA

Mali: Rais IBK azuru kijiji kilichokumbwa na mauaji cha Ogossagou

Ibrahim Boubacar Keita, rais wa Mali.
Ibrahim Boubacar Keita, rais wa Mali. © Sia KAMBOU / AFP

Siku mbili baada ya kijiji cha Ogossagou, katikati mwa Mali kukumbwa na shambulizi baya lililoua watu zaidi 130, rais wa nchi hiyo Ibrahim Boubacar Keita amezuru kijiji hucho.

Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yalitokea siku ya Jumamosi Machi 23. wakazi wa kijiji hicho wameyatoroka makaazi yao.

Katika shambulio hilo, mifugo iliteketezwa kwa moto, huku nyumba zikichomwa.

Rais Ibarahim Boubacara Keita amewasili katika eneo hilo kwa helikopta. Kiongozi wa kijiji hicho ambaye ni miongoni mwa watu waliouawa aliuawa mbele ya mke wake na kisha wauaji waliangamiza familia yote.

Wakati huo huo mbali kidogo na makazi ya kiongozi wa kijiji hicho, kumegunduliwa kaburi la halaiki ambapo inahofiwaa kuwa watu zaiinya arobaini walizikwa.

Rais wa Mali amezungumza na raia ambao tayari wamerejea katika makazi yao.

Siku ya Jumapili rais IBK alichukua uamuzi wa kuwaondoa wakuu wa jeshi kwenye nafasi zao na kuaamua kufuta kundi la wanamgambo la la Dan Nan Ambassagou.