MALI-MAUAJI-USALAMA

Mauaji Mali: Wakuu kadhaa wa jeshi waondolewa kwenye nafasi zao

Au moins une cinquantaine de personnes ont été tuées samedi dans l'attaque d'un village peul, dans le centre du Mali, le 23 mars 2019.
Au moins une cinquantaine de personnes ont été tuées samedi dans l'attaque d'un village peul, dans le centre du Mali, le 23 mars 2019. Google Maps

Kufuatia mauaji ya zaidi ya watu 135 kutoka jamii ya Fulani katikati mwa nchi ya Mali, karibu na mpaka na Burkina Faso, serikali ya nchi hiyo imetangaza kuvunja kundi la wanamgambo la Dan Nan Ambassagou" na kuwaondoa wakuu kadhaa wa jeshi kwenye nafasi zao.

Matangazo ya kibiashara

Siku moja baada ya mauaji hayo, pande mbalimbali zimeendelea kushtumiana, wakati zoezi la kuwahudumia waliojeruhiwa linaendelea.

Waziri Mkuu wa Mali amezungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha baraza la mawaziri na kutangaza kwamba "kundi la wanamgambo la Dan Nan Ambassagou", liloruhusiwa kumiliki silaha katikati mwa Mali, ambalo linadai kulindia usalama wakazi wa eneo hilo, limevunjwa.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mashirika kadhaa, kundi hilo linaundwa na wanamgambo wanaowafanyia vitendo vovu watu kutoka jamii ya Fulani. Vyanzo kadhaa vinajiuliza uwezekano wa wanamgambo hao kuhusika katika matukio ya Ogossagou, karibu na mji wa Bankass.

Katika hotuba yake, Waziri Mkuu wa Mali pia alionya kuwa "wanamgambo ambao hatakataa kutii amri ya kuweka chini silaha kwa hiari yao watapokonywa".

Zaidi ya watu 130 waliuawa na watu wenye silaha kwenye kijiji katikati mwa nchi ya Mali. Washambuliaji hao walikua wamevalia mavazi ya kijadi ya uwindaji.

Shambulio hilo lilijitokeza wakati mabalozi wa Umoja wa Mataifa walipokua nchini Mali kujadili ongezeko la machafuko nchini humo.

Mwaka uliopita, mamia ya watu waliuawa kwenye mapigano kati ya makabila mawili ya Dogon na Fulani.