DRC-RWANDA-USHIRIKIANO

Felix Tshisekedi na Paul Kagame waonyesha mshikamano wao wa ushirikiano

Rais Felix Tshisekedi (kushoto) na Paul Kagame katika Kongamano kuhusu fursa za kibiashara Afrika Machi Machi 26.
Rais Felix Tshisekedi (kushoto) na Paul Kagame katika Kongamano kuhusu fursa za kibiashara Afrika Machi Machi 26. Africa Ceo Forum

Rais wa DRC, Felix Tshiseked amemaliza ziara yake ya siku mbili nchini Rwanda. Felix Tshisekedi alipokelewa kwa shauku kubwa na mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya ziara ya siku mbili, ambayo iliingiliana na kongamano kiuchumi kuhusu fursa za kibiashara Afrika (Africa CEO Forum), wawili hao wakiwa pamoja walitangaza hadharani wakati wakuhitimisha kongamano hilo.

Walizungumzia kuhusu migogoro katika nchi zao na kuzungumzia kuhusu uchumi.

Baada ya mgogoro wa kidiplomasia uliofuata uchaguzi wa urais nchini DRC, mwenyeji wake Paul Kagame amesema "ana imani na ahadi ya Felix Tshisekedi kwa raia wake". Na kwa majirani zake: Kauli hiyo inakuja wakati Rwanda na Uganda zinapatia wakati mgumu wa mvutano.

Wakati huo huo rais wa DRC anataka kusuluhisha pande hizo mbili, akidai kuwa alikutana kwa mazungumzo na Paul Kagame na rais wa Uganda Yoweri Museveni, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi kuhusu mazungumzo yao.

Rais wa DRC pia alizungumzia kuhusu makundi mengi ya watu wenye silaha yaliyopo katika nchi yake, huku akiomba nchi jirani kusaidia nci yake ipat amani ya kudumu.

Mshikamano huu wa ushirikiano kati ya Rwanda na DRC pengine ikawa sababu japo bila kutajwa ikaifanya Rwanda kuweka nguvu za ushirikiano wa kibiashara na mataifa ya mbali kama vile Gabon na mengine ya kati na magharibi mwa Afrika.

Wiki iliyopita Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zilitia saini ya ushirikiano wa safari za anga ambapo ndege ya Rwanda, Rwandair itaanza safari za moja kwa moja baina ya Kigali na Kinshasa kuanzia April 15.