MSUMBIJI-MAFURIKO

Kimbunga Idai Msumbiji: Watu wakabiliwa na ugonjwa wa Kipindupindu

Miti, paa za nyumba, tani za plastiki vilipelekwa na na upepo na maji kufuatia kimbunga Idai nchini Msumbiji.
Miti, paa za nyumba, tani za plastiki vilipelekwa na na upepo na maji kufuatia kimbunga Idai nchini Msumbiji. ©Josh Estey/Care International via REUTERS

Hii ni mojawapo ya changamoto kubwa zinazokabili mji wa Beira katikati ya Msumbiji, eneo ambalo limeathiriwa zaidi na Kimbunga Idai. Imekuwa ni vigumu kudhibiti maelfu ya tani ya takataka ambazo kimbunga hicho kimesababisha.

Matangazo ya kibiashara

Mji wa Beira umetenga maeneo matatu ili kupokea takataka hizi zote. Mmoja ya maeneo hayo ni Ceramica, kilomita ishirini kutoka Beira.

Baadhi ya nyumba zimezungukwa na takataka.

Wakati huo huo mlipuko wa magonjwa ya kuambukia kama vile Kipindupindu vimeripotiwa katika baadhi ya maeneo nchini Msumbiji.

Shirika la Afya Duniani WHO limetuma dozi 900,000 kama chanjo ya ugonjwa wa Kipindupindu nchini humo.

Hii imekuja baada ya watalaam wa afya kuonya kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kutokea kwa kipindupindu kutokana na kimbunga kilichotokea nchini humo wiki iliyopita na kusababisha mamia ya watu kupoteza maisha na maelfu kuyatoroka makaazi yao.

Tayari watu watano wamethibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa Kipindupindu.

Hata hivyo baadhi ya watu wameanza kurejea katika baadhi ya maeneo hususan katika kijiji cha Praia Nova.

Wakaazi wa kijiji cha Praia Nova, nchini Msumbiji wameanza kurejea makwao baada ya kimbunga Idai.
Wakaazi wa kijiji cha Praia Nova, nchini Msumbiji wameanza kurejea makwao baada ya kimbunga Idai. ©Josh Estey/Care International via REUTERS