Pata taarifa kuu
COMORO-AU-SIAsa-USALAMA

Umoja wa Afrika watoa wito wa amani na utulivu Comoro

Rais mpya wa Comoro Azali Assoumani akiapishwa katika mji mkuu wa Comoro, Moroni Mei 26, 2016. (Picha ya zamani).
Rais mpya wa Comoro Azali Assoumani akiapishwa katika mji mkuu wa Comoro, Moroni Mei 26, 2016. (Picha ya zamani). © IBRAHIM YOUSSOUF / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Umoja wa Afrika unataka pande zinazotofautiana nchini Comoro kuwa watulivu na kuepeusha visa vinavyoweza kusababisha machafuko ya kisiasa.

Matangazo ya kibiashara

Hii inakuja baada ya upinzani katika Kiswa hicho, kukataa matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyompa ushindi rais Azali Assoumani, wakidai kuwa kulikuwa na wizi mkubwa.

Wiki jana vikosi vya usalama vya Comoro viliua watu watatu wenye silaha wakati wa urushianaji risasi karibu na kambi ya jeshi ya mji mkuu Moroni, kufuatia kutoroka kwa askari waasi gerezani.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mohamed Daoudou amebaini kwamba kundi la askari walioasi, ambao walikuwa wanazuiliwa jela kwa jaribio la mapinduzi la mwaka jana, walitoroka Alhamisi asubuhi na kwenda katika kambi ya jeshi kwa matumaini ya kuwashawishi askari kuwaunga mkono.

Azali Assoumani alitangazwa kuwa mshindi wa kiti cha rais baada ya uchaguzi wa Jumapili kwa 60% ya kura. Ujumbe wa waangalizi wa Afrika, ikiwa ni pamoja na ule wa Umoja wa Afrika (AU), ulihitimisha kuwa uchaguzi haukuwa wa kuaminika na wa wazi.

Tangu mwaka 1975 Comoro imeshuhudia mzozo wa kisiasa ikiwa ni pamoja na majaribio zaidi ya mapinduzi ya kijeshi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.