Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Algeria: Rais Abdelaziz Bouteflika kujiuzulu kabla ya Aprili 28

Abdelaziz Bouteflika, Julai 5, 2016, akizuru makaburi akitumia kiti cha magurudumu wakati wa maadhimisho ya miaka 57 ya uhuru wa Algeria.
Abdelaziz Bouteflika, Julai 5, 2016, akizuru makaburi akitumia kiti cha magurudumu wakati wa maadhimisho ya miaka 57 ya uhuru wa Algeria. © Canal / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika atajiuzulu "kabla ya Aprili 28," tarehe ambayo muhula wake utakuwa umemalizika, ofisi ya rais imetangaza kwenye taarifa yake. Rais wa Jamhuri anapaswa kuchukua "hatua za kuhakikisha kuendelea kwa utendaji kazi wa taasisi za serikali wakati wa kipindi cha mpito," taarifa hiyo imeongeza.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imekuja wakati Algeria inaendelea kukumbwa na maandamano kwa miezi kadhaa sasa. Waandamanaji wanaendelea kuandamana wakitaka rais Bouteflika na utawala wake waachie ngazi.

Hata hivyo baadhi wanampongeza Bouteflika kwa kazi nzuri aliyoifanya hasa kuimarisha usalama na mshikamano baina ya wananchi wa Algeria.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa kwenye vyombo vya habari vya serikali vya Algeria, kabla ya kujiuzulu Abdelaziz Bouteflika anataka "kuhakikisha mwendelezo wa utendaji kazi wa taasisi za serikali" wakati wa kipindi cha mpito. Kwa hiyo atachukua mfululizo wa hatua. Wakati huo wa mpito aliyotangaza mwanzoni mwa mwezi Machi, alipojiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais kwa muhula wa tano, ni kipindi ambacho kitatumiwa kwa marekebisho ya Katiba.

Kuondoka kwa rais ilikuwa mojawapo ya madai ya waandamanaji. Bouteflika anaamua kuachia ngazi kwa shinikizo la maandamano yaliyodumu wiki sita.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.