Pata taarifa kuu
MALI-CHAD-BURKINA FASO-BARKHANE-USALAMA

Kikosi cha askari wa Ufaransa, Barkhane, chapanua eneo lake la ulinzi

Kikosi cha askari wa Ufaransa (Barkhane) wakipiga doria Gossi.
Kikosi cha askari wa Ufaransa (Barkhane) wakipiga doria Gossi. © RFI / Olivier Fourt
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Kikosi cha askari wa Ufaransa kinachopambana na magaidi katika ukanda wa Afrika Magharibi (Barkhane) kimeamua kuongeza juhudi katika vita vyake dhidi ya makundi ya wanajihadi katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

"Muda umewadia wa kuongeza juhudi zetu" hadi katika eneo la Gourma, katikati na kaskazini mwa Mali, amesema Jenerali Frederic Blachon, kamanda wa kikosi cha askari wa Ufaransa (Barkhane) wanaopambana dhidi ya wanajihadi nchini Mali.

Kauli hiyo ameitoa katika mahojiano na shirika la Habari la AFP na RFI kutoka makao makuu ya kikosi hicho katika mji mkuu wa Chad N'Djamena.

Akiulizwa kuhusu tathmini ya shughuli za Barkhane katika mkoa wa Liptako nchini Mali na mambo muhimu ambayo wanatarajia kuyapa kipaumbele, Jenerali Blachon amejibu akisema kuwa kwa muda wa miezi kumi na nane wakiwa katika eneo hilo, walifanya kazi kubwa na kuhakikisha sasa usalama na amani vimerejea.

Hata hivyo amesema hilo halimaanishi kuwa adui ameangamizwa moja kwa moja, kuna uwezekano aendeshe mashambulizi ya kuvizia, au kutaka tu aonekane kama bado yupo, "lakini kwa uhakika ametokomezwa kabisa", amesema Jenerali Blachon

Ameahidi kuwa askari wake wataendelea na operesheni mbalimbali katika eneo la Liptako ili kuhakikisha kabisha wakaazi. "

Kwa sasa eneo hilo linaweza kudhibitiwa na idadi ndogo ya askari wetu", ameongeza Jenerali Blachon.

"Muda umewadia kupanua maeneo yetu ya usalama kwa maeneo mengine ambayo hutumika kama ngome ya makundi ya kigaidi yenye silaha. Tumeamua kupanua eneo hili hadi Gourma, kwenye mpaka na Burkina Faso. Maeneo haya ya mpakani ni maeneo ambayo makundi ya kigaidi yanatumia kwa kujificha na kufanya mashambulizi: amebaini Jenerali Blachon.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.