Pata taarifa kuu
LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Libya: Marshal Haftar aamuru majeshi yake kuingia Tripoli

Msafara wa magari ya kijeshi yakielekea Libya, Aprili 4, 2019.
Msafara wa magari ya kijeshi yakielekea Libya, Aprili 4, 2019. © Reuters TV via REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Majeshi ya Marshal Khalifa Haftar yanaendelea na mapigano karibu na mji mkuu wa Libya, Tripoli. Tayari majeshi hayo yamedhibiti miji miwili ya Sermane na Gheriane yanayopatikana mashariki na magharibi mwa Libya.

Matangazo ya kibiashara

Majeshi hayo yanasema yako tayari kuingia katika mji wa Tripoli, baada ya kupata agizo kutoka kwa kiongozi wao Marshal Kahalifa Haftar kuwataka waingie katika mji huo.

Makundi mbalimbali ya wanamgambo yako katika hali ya tahadhari na yanasema yako tayari kupambana.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kukutana haraka leo Ijumaa jioni ili kujadili hali hiyo.

Marshal Khalifa Haftar ameamua kutumia ufumbuzi wa kijeshi kwa Libya licha ya yote. Ameelezea mara kwa mara nia yake ya kuendesha mapigano hadi mji mkuu Tripoli katika miezi ya hivi karibuni, lakini kwanza ameamua kuendelea na vita katika eneo la kusini mwa nchi, labda kwa kulinda kundi la majeshi yake litakapoingia Tripoli.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.