Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Shambulio laua watu wawili Kaskazini mwa Nigeria

Kajuru, katika Jimbo la Kaduna, ambapo shambulio baya dhidi ya hoteli ya kifahari ya Kajuru Castle Resort, lilitokea siku ya Ijumaa, Aprili 19, 2019.
Kajuru, katika Jimbo la Kaduna, ambapo shambulio baya dhidi ya hoteli ya kifahari ya Kajuru Castle Resort, lilitokea siku ya Ijumaa, Aprili 19, 2019. © Google Maps
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Watu wawili, ikiwa ni pamoja na mfanyakazi wa shirika la misaada kutoka Uingereza, wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wenye silaha. Shambulio hilo lilitokea siku ya Ijumaa (Aprili 19), na watalii wanne walitekwa nyara na watu wenye silaha katika hoteli kaskazini mwa Nigeria, polisi imesema leo Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi ya Ijumaa yalilenga hoteli ya kifahari ya Kajuru Castle Resorilijengwa kwenye mlima karibu kilomita 60 kutoka mji wa Kaduna kaskazini mwa Nigeria.

Watu kadhaa wenye silaha walijaribu kuivamia hoteli hiyo. Mfanyakazi mwanamke wa shirika la misaada kutoka Uingereza na raia mmoja wa Nigeria aliyekuwa pamoja naye walipigwa risasi, wakati watalii wanne wa Nigeria kutoka kundi la watu kumi na tatu waliokuwa wamewasili muda si mrefu jijini Lagos, mji mkuu wa kiuchumi wa Nigeria, waliteka nyara.

Raia huyo wa Uingereza, Faye Mooney, alikuwa mfanyakazi wa shirika la kimataifa linalotoa misaada la Mercy Corps, ambalo limethibitisha kifo chake jana Jumapili Aprili 21.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.