Pata taarifa kuu
DRC-MONUSCO-SIASA-USALAMA

Monusco yajiandaa kufunga ofisi zake kadhaa DRC

Monusco imeweka nguvu zake nyingi katika maeneo ambayo kunaripotiwa kundi mengi ya watu wenye silaha, kama hapa Kaskazini mwa mkoa wa Kivu Kaskazini.
Monusco imeweka nguvu zake nyingi katika maeneo ambayo kunaripotiwa kundi mengi ya watu wenye silaha, kama hapa Kaskazini mwa mkoa wa Kivu Kaskazini. © ALEXIS HUGUET / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC MONUSCO imeanza mchakato wa kufunga ofisi zake kadhaa nchini DRC, hasa Magharibi mwa nchi hiyo. Ofisi nane zinatarajiwa kufungwa mwishoni mwa mwezi Juni. Pia Monusco inatarajia kupunguza bajeti mpya, mchakato ambao utaanza Julai 1.

Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (Monusco) unapanga kufuta nafasi 6,700, ambapo robo tatu ya nafasi hizo zinashikiliwa na raia wa DRC. Hata hivyo hatua hiyo itahusua wafanyakazi wa kiraia kutoka kitengo cha haki za binadamu, masuala ya kisiasa na mawasiliano. Hatua hiyo haihusu askari.

Ofisi nane ambazo kzinatarajiwa kufungwa ifikapo Juni 30 ni ofisi za Umoja wa Mataifa Dungu, Mbandaka, Bandundu, Kamina, Matadi, Mbuji-Mayi, lakini pia Kisangani na hatimaye Lubumbashi, mji wa pili kwa ukubwa ambao unakabiliwa na mdororo wa usalama katika miezi ya hivi karibuni.

Wakati huo huo Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, Leila Zerrougui, amesema kuwa anaamini kuwa rais mpya wa Jamhuri ya kdiemokrasia ya Congo, Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo, ameonesha utashi wa kisiasa, na nia njema kuliongoza taifa hilo kubwa, hali ambayo inapaswa kuungwa mkono na wote nchini humo.

Zerrougui, aliyaesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu wiki hii jijini Kinshasa, ambapo aliongeza kuwa Monusco itafanya kila jitihada kuhakikisha kiongozi huyo anafanikiwa katika mipango aliyo nayo kuinua uchumi, na kuboresha maisha ya wananchi wa taifa hilo tajiri, lakini raia wake wakiendelea kubaki masikini.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.