Pata taarifa kuu
DRC-AJALI-USALAMA

Ajali ya Boti Kalehe: Miili 37 yaokolewa katika Ziwa Kivu

Maafisa wa shirika la Msalaba Mwekundu kutoka DRC na Rwanda wakiokoa miili iliyopatikana katika Ziwa Kivu kwenye pwani ya Gisenyi Aprili 20, 2019.
Maafisa wa shirika la Msalaba Mwekundu kutoka DRC na Rwanda wakiokoa miili iliyopatikana katika Ziwa Kivu kwenye pwani ya Gisenyi Aprili 20, 2019. ALEXIS HUGUET / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Miili thelathini na saba ya watu wanaosadikiwa kuwa walipoteza maisha katika ajali ya boti iliyozama aprili 9 huko mashariki mwa DRC imepatikana, maafisa wakuu wa serikali wamesema Jumanne wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Gavana wa jimbo la Maniema,Papy Omeonga Tchopa, kwa shirika la habari la la AFP Jumanne wiki hii ni kuwa mbali na miili hiyo 37 iliyopatikana ikielea juu ya Ziwa Kivu, manusura kumi na sita walijikuta ufukweni karibu na eneo ilikotokea ajali hiyo aprili 9 mwaka huu.

Omeonga Tshopa pia ameongeza kuwa boti hiyo ilizama karibu na kijiji cha Katalama, kilichoko kwenye umbali wa kilomita 120 kutoka Kindu, mji mkuu wa mkoa huo wa maniema, kati ya eneo la Kibombo na Kasongo, eneo ambalo ni marufuku kwa meli ya aina yoyote kusafiria.

Ajali za boti zimekuwa zikishuhudiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika siku za hivi karibuni, huku wadadisi wa mambo wakihoji kuhusu safari za majini kwa kutumia vyombo chakavu ambavyo vimehudumu kwa muda wa miaka mingi bila kufanyiwa uchunguzi wala marekebisho.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.