SUDAN-JESHI-MAANDAMANO-BASHIR-SIASA

Maandamano zaidi yaitishwa Sudan kupinga hatua ya jeshi kukawia kukabidhi madaraka kwa raia

Waandamanaji wakiwa na bango la rais aliyeondolewa madarakani Omar Al Bashir
Waandamanaji wakiwa na bango la rais aliyeondolewa madarakani Omar Al Bashir ©REUTERS/Umit Bektas

Maandamano makubwa zaidi yanatarajiwa nchini Sudan, wakati huu waandamanaji wakidai kuwa jeshi la nchi hiyo halioneshi utashi wa kuwa tayari kukabidhi madaraka kwa raia.

Matangazo ya kibiashara

Wito wa maandamano umetolewa wakati huu viongozi wa waandamanaji na wanajeshi wakivutana kuhusu muundo wa baraza la kijeshi, ambapo mwishoni mwa juma lililopita, walikubaliana lijumuishe raia.

Jeshi kwa upande wake limesisitiza utayari wa kukabidhi madaraka kwa raia lakini baada ya kupatikana kwa muafaka.