DUNIA-KAZI-JAMII

Ulimwengu waadhimisha siku ya kimataifa ya wafanyakazi

Wafanyakazi kote duniani, wanaadhimisha siku hii kwa kusherehekea mafanikio yao lakini pia kuangazia changamoto zinazowakumba katika maeneo ya kazi.

Wafanyakazi wa Afrika Kusini wakiendelea na mgomo wao kwenye barabara ya Johannesburg Septemba 2, 2010, ili waweze kupata ongezeko la mshahara.
Wafanyakazi wa Afrika Kusini wakiendelea na mgomo wao kwenye barabara ya Johannesburg Septemba 2, 2010, ili waweze kupata ongezeko la mshahara. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi hutumia siku kama ya leo kuwataka waajiri kuwaongezea wafanyakazi mshahara na kuboresha mazingira ya kufanya kazi.

Ni siku ambayo inaadhimishwa pia katika mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.

Wafanyakazi kwenye ukanda wa nchi za Afrika Mashariki wameendelea kukabiliwa na changamoto ikiwemo mazingira mabaya ya kufanyika kazi na mishahara duni.

Siku hii imefika wakati ambapo katika mataifa mengi kunashuhudiwa mfumuko wa bei za chakula, huku mshahara ukisalia pale pale.

Wafanyakazi katika sekta ya umma na ile binafsi wamekua wakilalamikia mishahara duni, huku wakiomba kuongezwa mishahara kutoka na hali ya maisha inayoendelea.

Kumekua na maandamano ya hapa na pale kufuatia madai ya wafanyakazi kuhusu mshahara wakisema mshahara wanaopewa haikidhi mahitaji yao ya kila siku.