EBOLA-DRC-WHO

Visa 26 vya ebola vyaripotiwa kila siku DRC

Watu 26 wamethibitishwa kufa ndani ya siku moja kwenye jimbo la Kivu Kaskazini kutokana na maradhi ya ugonjwa wa Ebola unaoendelea, kusumbua nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wafanyakazi wa taasisi ya msalaba mwekundu wakibeba jeneza la mgonjwa aliyefariki kwa maradhi ya ebola
Wafanyakazi wa taasisi ya msalaba mwekundu wakibeba jeneza la mgonjwa aliyefariki kwa maradhi ya ebola REUTERS/Baz Ratner/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko wa sasa ni wa pili mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa baada ya ule uliokumba maeneo ya Afrika Magharibi mwaka 2014-2016 na kuua watu zaidi ya elfu 11.

Wizara ya afya nchini DRC imethibitisha vifo vya watu 957 huku ikirekodi visa vya watu 891 ambao wanamaambukizi.

Serikali imetangaza mikakati zaidi ya kukabiliana na kuenea kwa maambukizi zaidi kama anavyoeleza hapa Daktari Jean Jacques Muyambo.

Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola mashariki mwa DRC yameendelea kuwa magumu kutokana na makundi ya waasi kushambulia vituo vya afya vinavyotoa matibabu kwa wagonjwa wa Ebola.