BENIN-SIASA-UCHAGUZI
Wananchi wa benin wasubiri matokeo ya uchaguzi wa rais
Wananchi wa Benin wanaendelea kusubiri kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita, uchaguzi ambao kwa mara ya kwanza umeshuhudia idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Wakati huu kukiwa hakuna muda maalumu wa kutangazwa kwa matokeo rasmi, taarifa kutoka ndani ya tume ya uchaguzi zinasema huenda yakaanza kutangazwa Alhamisi hii.
Upinzani nchini humo umeendelea kupinga mchakato wa uchaguzi ulivyokuwa na kutoa wito wa matokeo hayo kufutwa.
Uchaguzi wa Jumapili, umefanyika bila ya kuwepo kwa mgombea yeyote wa upinzani.