Umoja wa Afrika watishia kuchukua vikwazo dhidi ya jeshi Sudani

"Tuko tayari kuzungumza, lakini kuanzia sasa hatutaki vurugu," amesema Mohammed Hamdan Dagalo, naibu kiongozi wa Baraza la Jeshi la Mpito (TMC) Khartoum, Aprili 30, 2019.
"Tuko tayari kuzungumza, lakini kuanzia sasa hatutaki vurugu," amesema Mohammed Hamdan Dagalo, naibu kiongozi wa Baraza la Jeshi la Mpito (TMC) Khartoum, Aprili 30, 2019. ASHRAF SHAZLY / AFP

Siku chache baada ya muda wa siku 30 kupita bila ya jeshi la Sudan kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia, umoja wa Afrika umeongeza siku 60 kwa jeshi hilo kufanya hivyo au likabiliwe na vikwazo.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Afrika umetishia kusitisha uanachama wa nchi hiyo ikiwa wanajeshi hawatakabidhi madaraka kwa raia, AU imetoa imelitaka jeshi kuondoka madarakani kuanzia April 15.

Katika hatua nyingine kinara wa upinzani nchini Sudan, Sadiq al-Mahdi amewataka waandamanaji kutowachokoza wanajeshi kwa kuwa watakabidhi madaraka hivi karibuni.

Waandamanaji wanaendelea kupiga kambi mbele ya makao makuu ya jeshi licha ya Omar Hassan al-Bashir kuachia ngazi, wakiomba jeshi kukabishi madaraka kwa raia.