UTURUKI-LIBYA-USALAMA

Uturuki: Raia wetu wawili wanaoshikiliwa Libya sio majasusi

Maofisa usalama wa Uturuki wamekanusha taarifa kuwa raia wake wawili waliokamatwa na vikosi vya mbabe wa kivita nchini Libya, Jenerali Khalifa Haftar ni majasusi.

Wakaazi wa viunga vya mji wa tripoli wanaendelea kuyatoroka makaazi yao kufuati mapigano makali kati ya majeshi ya serikali na yale ya Marshal Khalifa Haftar.
Wakaazi wa viunga vya mji wa tripoli wanaendelea kuyatoroka makaazi yao kufuati mapigano makali kati ya majeshi ya serikali na yale ya Marshal Khalifa Haftar. REUTERS/Hani Amara
Matangazo ya kibiashara

Wafanyakazi hao waliokuwa wanafanya kazi kwenye mgahawa mmoja mashariki mwa mji unaokaliwa na wanajeshi wa Haftar, walikamatwa April 12 kwenye wilaya ya Ghashir wakituhumiwa kwa ujasusi.

Katika hatua nyingine kiongozi mmoja wa kundi la wapiganaji waliokuwa wanaiunga mkono Serikali ya Tripoli Meja Jenerali Omar Abdel Jalil ametangaza kumuunga mkono Jenerali Haftar.

Haya yanajiri wakati huu kukiendelea kuripotiwa mapigano makali nje kidogo ya mji wa Tripoli kati ya wanajeshi wa Serikali na wale wa Jenerali Haftar.