DUNIA-VYOMBO VYA HABARI-USALAMA

RSF: Tuna wasiwasi kuhusu uhuru wa Vyombo vya Habari Afrika

Wakati Ijumaa wiki hii dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, jumla ya waandishi wa habari 95 waliuawa mwaka uliopita na hii ni kwa mujibu wa shirikisho la kimataifa la wanahabari IFJ.

Katika nchi za Morocco, Comoro, Guinea, DRC na Burundi, uhuru wa vyomo vya Habari uko mashakani, kwa mujibu wa RSF (picha kumbukumbu).
Katika nchi za Morocco, Comoro, Guinea, DRC na Burundi, uhuru wa vyomo vya Habari uko mashakani, kwa mujibu wa RSF (picha kumbukumbu). © Siegfried Forster / RFI
Matangazo ya kibiashara

Siku hii inaadhimishwa huku dunia ikishuhudia waandishi wa habari wakiendelea kuuawa, kupokea vitisho, kuteswa , kupotezwa na hata kutekwa kwenye maeneo mbalimbali duniani.

Bara la Afrika ni miongoni mwa maeneo yanayotajwa kuwa hatari zaidi kwa waandishi wa habari kufanya kazi huku ikishuhudiwa vyombo vingi vikifungwa au kupokea vitisho.

Siku ya Kimataifa ya kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya Habari
Siku ya Kimataifa ya kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya Habari RFI-KISWAHILI

Kwa upande wake shirika la waandishi wa habari wasio na mipaka RSF, lenyewe linaonya dhidi ya Serikali zinazominya uhuru wa habari, likitolea mfano hali inayoshuhudiwa nchini Burundi.