DRC-USALAMA

Waasi zaidi ya sita wauawa katika mapigano na vikosi vya jeshi DRC

Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006.
Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006. REUTERS

Wapiganaji 6 wa waasi wameripotiwa kuuawa mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika makabiliano na wanajeshi wa Serikali (FARDC).

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini DRC, kundi la waasi waliokuwa na silaha walivamia kijiji kimoja kwenye jimbo la Ituri na kuua watu sita huku kukiwa na hofu kuwa mamia ya raia wametekwa.

Msemaji wa jeshi la DRC amelaani shambulio hilo linalodaiwa kutekelezwa na wapiganaji wa kundi la ADF.

Taarifa zaidi zinasema kuwa wanajeshi wa Serikali walikabiliana na waasi hao kwa zaidi ya saa moja kabla ya kuwashinda nguvu ambapo wameripoti kuwaua wapiganaji zaidi ya 6.

Kiongozi mmoja wa kijadi kwenye eneo hilo amesema mpaka sasa watu 30 hawajulikani walipo na wanahofu kuwa huenda walitekwa nyara na waasi hao huku zaidi ya ngombe 100 pia wakichukuliwa.