DRC-AJALI-USALAMA

Ajali za boti zaendelea kusababisha vifo DRC

Ajali ya hivi karibu iliyouwa wengi mashariki mwa DRC ilitokea katika Ziwa Kivu (kwenye picha), katika eneo la Kalehe.
Ajali ya hivi karibu iliyouwa wengi mashariki mwa DRC ilitokea katika Ziwa Kivu (kwenye picha), katika eneo la Kalehe. Photo MONUSCO/Force

Watu wawili wamepoteza maisha na wengine kuzama baada ya boti waliokuwa wanasafiria kuzama katika kisiwa cha Tshegera katika Ziwa Kivu, Mashariki mwa Jamhuri ay Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Boti hiyo ilikuwa inatokea katika kijiji cha Butumba kwenda katika soko la Kituku mjini Goma, wakati ilipozama.

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa abiria na mizigo kupita kiasi na hali mbaya ya hewa zimesababisha ajali hiyo.

Mwezi uliopita, watu zaidi ya mia moja walipoteza maisha baada ya boti nyingine kuzama.