LIBYA-UFARANSA-USHIRIKIANO

Libya: Ufaransa yathibitisha kumuunga mkono Fayez el-Sarraj

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amethibitisha "uungwaji mkono wa Ufaransa kwa kiongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya (GNA) Fayez el-Sarraj, ambaye alipokelewa Jumatano, Mei 8 katika ikulu ya Elysee.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amempokea Waziri Mkuu wa Libya Fayez-al-Sarraj katika ikulu ya Elysee Mei 8, 2019.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amempokea Waziri Mkuu wa Libya Fayez-al-Sarraj katika ikulu ya Elysee Mei 8, 2019. © REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Ufaransa imezitaka pande zinazohasimiana nchini Libya kusitisha mapigano haraka iwezekanavyo.

Emmanuel Macron "amethibitisha uungwaji mkono wa Ufaransa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, ambayo Ufaransa itaendelea na ushirikiano wake," ikulu ya Elysee imesema katika taarifa.

Rais wa Ufaransa "amehimiza pande zote zinazopigana nchini Libya kusitisha mapigano bila masharti" baada ya mashambulizi kabambe yaliyozinduliwa mapema mwezi Aprili na majeshi ya Marshal Haftar, yanayodhibiti eneo la mashariki mwa nchi. Rais Macron amependekeza "maeneo ambayo vita vinapaswa kukomeshwa, chini ya usimamizi wa kimataifa, ili kufafanua mfumo sahihi," ikulu ya Elysee imeongeza.

Viongozi hawa wawili walikubaliana juu ya umuhimu wa kuwashirikisha wadau wote katika mazungumzo kutoka mashariki, kusini na magharibi mwa nchi, ikiwa ni pamoja na mashirika ya kiraia, " Elysee imebaini.

Serikali ya Fayez el-Sarraj, inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa, hivi karibuni ilishutumu Ufaransa kumsaidia Marshal Haftar katika mashambulizi dhidi ya mji wa Tripoli. Mkutano huo, ulikuwa na lengo la kujieleza kuhusu shutma hizo za serikali ya Tripoli ambazo Ufaransa inakanusha na kusema kuwa shutma hizo hazina na msingi.

Kwa pendekezo la kusitisha mapigano, Fayez el-Sarraj na serikali yake wamekataa hadi sasa makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano kabla ya kuondolewa kwa askari wa Haftar kwenye ngome walizoshikilia baada ya mashambulizi, mashariki na kusini mwa nchi.