SUDAN-JESHI-MAANDAMANO-BASHIR-SIASA

Jeshi na viongozi wa waandamanaji kuzungumza tena

Mwezi mmoja baada ya kuondolewa madarakani kwa rais wa Sudan Omar Al Bashir, maelfu ya waandamanaji bado wamepiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi jijini Khartoum, wakishinikiza serikali ikabidhiwe kwa raia.

Waandamanaji nchini Sudan wakiwa mbele ya makao makuu ya jeshi jijini Khartoum
Waandamanaji nchini Sudan wakiwa mbele ya makao makuu ya jeshi jijini Khartoum Photo: Ashraf Shazly/AFP
Matangazo ya kibiashara

Jeshi limesalia madarakani tangu Aprili 11 baada ya kuondoka kwa Bashir na kuzuiwa kwa mujibu wa ripoti za kijeshi.

Waandamanaji kwa upande wao, wamegoma kurejea nyumbani, wanasema wataendelea kushinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.

Kufikia malengo yao, viongozi waaandamanaji wameitisha mgomo wa siku nzima kuanzia siku ya Jumatatu.

Hata hivyo, ripoti kutoka Khartoum zinasema  kuwa mazungumzo mapya yanatarajiwa kufanyika kuhusu kuona uwezekano wa jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.

Viongozi wa waandamanaji wanasema, wangepanda kumaliza mazungumzo hayo na suluhu kupatikana ndani ya saa 72 zijazo.