AFRIKA KUSINI-UCHAGUZI-RUSHWA-SIASA

Ramaphosa aahidi kutokomeza rushwa

Cyril Ramaphosa akicheza mbele ya wafuasi wake, Johannesburg, Mei 12, 2019.
Cyril Ramaphosa akicheza mbele ya wafuasi wake, Johannesburg, Mei 12, 2019. REUTERS/Mike Hutchings

Baada ya ushindi wa chama cha ANC katika Uchaguzi Mkuu nchini Afrika Kusini, Rais Cyril Ramaphosa na wafuasi wake wameendelea kusherehekea ushindi huo.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha ANC, madarakani tangu mwaka 1994, kimeshinda uchaguzi kwa 57.5% ya kura katika ngazi ya kitaifa.

Mbele ya umati wa wafuasi wake, kwenye makao makuu ya chama cha ANC "Luthuli House", rais Ramaphosa amewashukuru wapiga kura ambao wamemwamini. Lakini amesema anasikitishwa kuona chama chake kinaendelea kupoteza umaarufu katika miji kadhaa na kupoteza kura nyingi hadi kupata chini ya 60% ya kura katika uchaguzi mkuu.

Rais Ramaphosa amesema ulikuwa ni uchaguzi mgumu kwao lakini wamejifunza mengi wakati huu wakirejea madarakni kwa wabunge pungufu.

Hata hivyo Ramaphosa amesema sasa nchi yake inafungua ukurasa mpya, huku akiahidi kupambana dhidi ya vitendo vya rushwa na kuhakikisha rushwa inatokomezwa nchini.