DRC-FAYULU-SIASA

Fayulu aapa kuendelea na mapambano kuhusu "ukweli wa matokeo ya uchaguzi

Kiongozi wa upinzani nchini DRC, Martin Fayulu anasema yuko tayari "kuendelea" na mapambano kuhusu "ukweli wa matokeo ya uchaguzi" nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Martin Fayulu, baada ya kuwasilisha malalamiko yake mbele ya Mahakama ya Katiba dhidi ya matokeo ya uchaguzi wa urais, Januari 12, 2019.
Martin Fayulu, baada ya kuwasilisha malalamiko yake mbele ya Mahakama ya Katiba dhidi ya matokeo ya uchaguzi wa urais, Januari 12, 2019. © REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Martin Fayulu, ambaye anaendelea kupinga uchaguzi wa Felix Tshisekedi kwenye nafasi ya rais wa jamhuri, amerejelea kauli hiyo Jumatatu, Mei 13 mjini Kinsangani ambako alifanya mkutano na wafuasi wake, ikiwa ni mkutano wa kwanza nje ya Kinshasa tangu arejee DRC. Katika mji wa Kisangani ndipo ambapo Martin Fayulu aliweza kukusanya idadi kubwa ya watu wakati wa kampeni zake mikoani.

Alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kisangani, Fayulu alipokelewa na umati wa wafuasi wake na kuongozana nao hadi kwenye eneo la Posta ambapo alifanya mkutano wake huo.

Katika ziara hiyo, Fayulu aliongozana na Eve Bazaïba wa chama cha MLC cha Jean-Pierre Bemba na Adolphe Muzito.

Martin Fayulu amewataka wananchi wa DRCongo kufanya waliwezalo ili kuvunja uhusiano kati ya Felix Tshisekedi na rais wa zamani Joseph Kabila.