UBELGIJI-DRC-SIASA-DIPLOMASIA

DRC na Ubelgiji zinajadiliana kurejesha uhusiano uliovunjika mwaka 2018

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Ubelgiji zinajadiliana kurejesha upya mahusiano ya kidiplomasia yaliyokuwa yamevunjika tangu mwezi Januari mwaka 2018.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi akisalimiana na Mjumbe maalum wa Ubelgiji katika eneo la Maziwa Makuu, Renier Nijskens Mei 14 2019
Rais wa DRC Felix Tshisekedi akisalimiana na Mjumbe maalum wa Ubelgiji katika eneo la Maziwa Makuu, Renier Nijskens Mei 14 2019 Radio Okapi
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya rais mjini Kinshasa imesema rais Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo amekuwa na mazungumzo ya kina na ujumbe wa pamoja unaongozwa na Mjumbe maalum wa Ubelgiji katika eneo la Maziwa Makuu, Renier Nijskens.

Brussels imesema iko tayari kurejesha ushirikiano wa kijeshi kati yake na DRC, pamoja na kuhakikisha unaboreshwa mfumo wa utoaji wa visa za mataifa ya Ulaya ya Schengen.

Aidha, Ubelgiji imeahidi kuwa safari za ndege kati ya Brussels na Kinshasa zitarejea kama kawaida.

Uhusiano kati ya DRC na mkoloni wake Ubelgiji uliingia doa mwaka 2018, kwa sababu za kisiasa wakati Brussels ilipoamua kumwekea shinikizo raia wa zamani Jospeh Kabila asiwanie tena urais.