DRC-SIASA-DIPLOMASIA-UBELGIJI-UFARANSA

Rais Tshisekedi aendeleza harakati za kidiplomasia

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi ameendelea na harakati za kidiplomasia kuimarisha uhusiano wa nchi yake na mataifa ya nje.

Rais wa DRC  Félix Tshisekedi
Rais wa DRC Félix Tshisekedi SIMON MAINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wiki ijayo, Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian atazuru jijini Kinshasa kukutana na raisTshisekedi, kujadili uhusiano wa nchi hizo mbili.

Hatua hii inakuja, baada ya wiki hii, Tshisekedi kukutana na wawakilishi wa serikali ya Ubelgiji na kuahidi ushirikiano mpya wa kidiplomasia kati ya Kinshasa na Brussels.

Kukutana kwa rais Tshisekedi na Renier Nijskens mjumbe wa Ubelgiji katika eneo la Maziwa Makuu, linatoa matumaini kwa kuimarika tena kwa uhusiano wa nchi hizo mbili, baada ya uhusiano kuvunjika mwaka 2018.

Wiki iliyopita, kiongozi huyo wa DRC pia alikutana na Mkuu wa Majeshi nchini Rwanda, Patrick Nyamvumba.

Tshisekedi, amezuru Marekani, Kenya, Angola miongoni mwa mataifa mengine jirani kama Rwanda na Uganda.