AFRIKA-TEKNOLOJIA-RWANDA

Viongozi wa Afrika wahimizwa kukubali matumizi ya teknolojia

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, rais wa Rwanda Paul Kagame na Ibrahim Keita wa Mali wakiwa jijini Kigali Mei 15 2019
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, rais wa Rwanda Paul Kagame na Ibrahim Keita wa Mali wakiwa jijini Kigali Mei 15 2019 The New Times

Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta, wanatoa wito kwa viongozi wenzao barani Afrika kukumbatia teknolojia kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Wakihudhuria kongamano jijini Kigali pamoja na rais wa Mali Ibrahim Boubakar Keita, wamehimiza mataifa ya Afrika kuwekeza zaidi katika teknolojia.

“Teknolojia mfano ya mawasiliano imekuwa kama safaro ya ndege.Ninapompigia simu rais Kenyatta huko Kenya au Mali, sauti yangu lazima iende hadi Ulaya ndio imfikie, hatuwezi kuendelea hivi,” alisema rais Kagame.

Rais Kenyatta amesema mataifa ya Afrika yana jukumu la kutumia teknolojia vema kwa matumizi ya maendeleo na sio kutumia teknlojia kwa ajili ya kuhubiri chuki, mgawanyiko ili kutatua changamoto mbalimbali.