DRC-SIASA-WAZIRI MKUU-TSHISEKEDI

Rais Tshisekedi kumtaja Waziri Mkuu wiki ijayo

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amesema kuwa Waziri Mkuu mpya atafahamika wiki ijayo.

Rais wa DRC  Félix Tshisekedi
Rais wa DRC Félix Tshisekedi Stringer/AFP
Matangazo ya kibiashara

Tshisekedi ametoa hakikisho hilo wakati akikutana na Mabalozi wa umoja wa Ulaya na yule kutoka Canada jijini Kinshasa siku ya Jumamosi.

Hili pia limethibitishwa na msemaji wa rais Tshisekedi, Kasongo Mwema Yamba Y'amba, kupitia ukurasa wake wa Twiter, ambaye ameandika kuwa rais Tshisekledi amewaambia balozi hao kuwa, Waziri Mkuu amepatikana.

Wananchi wa DRC wanasubiri kuona ni atakuwa Waziri Mkuu kwa sababu kwa mujibu wa katiba anastahili kutokea kwenye chama chenye wabunge wengi na kwa sasa muungano wa kisiasa wa rais wa zamani Joseph Kabila ndio ulio na wabunge wengi.

Tangu alipoingia madarakani mapema mwaka huu rais Tshisekedi hajafanikiwa kuunda serikali yake.