DRC-EBOLA-AFYA-WHO

WHO: Kudhibiti maambukizi ya Ebola Mashariki mwa DRC inakuwa ngumu

Shirika la afya duniani WHO linasema maafisa wa afya Mashariki mwa DRC bado wanakabiliwa na changamoto nyingi katika jitihada za kudhibiti maambukizi mapya ya ugonjwa hatari wa Ebola.

Mazishi ya mtu aliyeambukizwa Ebola Mashariki mwa DRC
Mazishi ya mtu aliyeambukizwa Ebola Mashariki mwa DRC REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Daktari Michael Ryan Mkurugenzi anayehusika na masuala ya dharura katika Shirika hilo amekuwa akizuru Butembo, amesema changamoto kubwa ni utovu wa usalama.

Ametoa mfano wa maafisa wa afya kuvamiwa hivi karibuni wakati wakienda kumzika mtu aliyekuwa amepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo, suala ambalo amesema itakuwa ni vigumu kupambana na Ebola.

Tangu mwezi Agosti mwaka 2018, watu 1161 wamepoteza maisha Mashariki mwa nchi hiyo huku wengine zaidi ya 1,600 wakiambukizwa.

WHO inaonya kuwa iwapo hali hii itaendelea kushuhudiwa, kuna hatari kubwa ya ugonjwa huo kusambaa katika nchi jirani.