SUDAN-JESHI-MAANDAMANO-BASHIR-SIASA

Mazungumzo kati ya waandamanaji na viongozi wa kijeshi yaendelea

Majadiliano zaidi kati ya viongozi wa kijeshi na wale wa waandamanaji nchini Sudan yanatarajiwa kuendelea leo ikiwa ni uhitimishwaji wa muundo mpya wa baraza litakalotawala, pande hizo mbili zimethibitisha baada ya saa kadhaa za majadiliano ambayo hayakufikia makubaliano.

Waandamanaji nchini Sudan
Waandamanaji nchini Sudan Photo: AFP
Matangazo ya kibiashara

Pande zote mbili zimekuwa zikitaka ushiriki kikamilifu katika baraza jipya litakalotawala Sudan kwa miaka mitatu ya mpito baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa muda mrefu Omar El Bashir.

Majadiliano ya hivi karibuni yaliyofanyika Jumapili yalifuatia shinikizo kutoka kwa mataifa yenye nguvu duniani kuundwa kwa baraza la kiraia litakalotawala,ambalo ndio moja kati ya matakwa muhimu ya waandamanaji.

Luteni Jenerali Shamseddine Kabbashi,ambaye ni msemaji wa baraza la kijeshi, aliwaambia waandishi wa habari kuwa kilichojadiliwa ni Mfumo wa mamlaka huru.

Shirikisho la Maprofesa wa vyuo vikuu nchini sudan ambalo lilianzisha kampeni ya maandamano dhidi ya Bashir mwezi Desemba, lilisema kuwa halina haraka ya kuhitimisha makubaliano hayo.