DRC-UFARANSA-SIASA-TSHISEKEDI-DIPLOMASIA

Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa Jean Yves le Drian kuzuru DRC

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Jean Yves le Drian ambaye aliwahi kupinga ushindi wa DRC Felix Tshisekedi  anatarajiwa jijini Kinshasa siku ya Jumatatu katika ziara ya kikazi. 

Rais wa Ufaransa  Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Akiwa jijini Kinshasa, le Drian anatarajiwa kukutana na kushauriana na rais Felix Tshisekedi ambaye amekuwa madarakani tangu mwezi Januari.

Ziara hii inakuja wakati huu kiongozi huyo wa DRC akiendeleza harakati za kidiplomasia kuomba uungwaji mkono kutoka kwa mataifa ya kigeni.

Tangu alipoingia madarakani, rais Tshisekedi, ametembelea mataifa karibu yote katika ukanda wa Maziwa Makuu lakini pia amewahi kwenda nchini Marekani.

Ufaransa ambayo inaisaidia  DRC kutoa mafunzo ya polisi wake, na sekta ya afya miongoni mwa nyingine inapanga tena kumsaidia rais mpya wa nchi hiyo.

Ujio huu wa Jean-Yves Le Drian unalenga kudumisha uhusiano wa Kinshasa na Paris wakati huu nchi hiyo ikiendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama na ugonjwa wa Ebola Mashariki mwa nchi hiyo.