MALAWI-SIASA-UCHAGUZI-WABUNGE-URAIS

Mamilioni wapiga kura nchini Malawi kumchagua rais na wabunge

Malawi inafanya uchaguzi wake mkuu siku ya Jumanne, baada ya kampeni zilizokuwa na ushindani mkali kati ya rais Peter Mutharika anayetetea kiti chake dhidi ya mahasimu wawili ambao ajenda zao kuu imekuwa maendeleo ya kiuchumi na kupambana na ufisadi.

Wananchi wa Malawi wapiga kura Mei 21 2019
Wananchi wa Malawi wapiga kura Mei 21 2019 MBC
Matangazo ya kibiashara

Mutharika, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2014,atakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa aliyekuwa naibu wake Saulos Chilima na mhubiri wa zamani wa Lazarus Chakwera.

''Tumeiweka Malawi katika uelekeo wa maendeleo''alisikika Mutharika, mwenye umri wa miaka 78, akiwaambia maelfu ya wafuasi wa chama chake DPP mjini Blantaya akihitimisha kampeni zake mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kuwania kwake muhula wa pili kumejikita katika ajenda ya uchumi na rekodi zake za kuimarisha miundo mbinu za barabara na umeme katika eneo la kusini mashariki mwa nchi.

Wapiga kura nchini Malawi Mei 21 2019
Wapiga kura nchini Malawi Mei 21 2019 MBC

Chini ya utawala wa Mutharika, mfumuko wa bei umeshuka kutoka asilimia 23 hadi chini ya asilimia tisa, lakini bado asilimia 11 tu ya watu ndio wanapata umeme.

Uchaguzi huu ni wa kwanza tangu kuanzishwa sheria mpya inayohimiza vyama kutangaza mchango mkubwa na kupiga marufuku mazoea ya wagombea wa kutoa fedha kwa raia.

Wapiga kura Milioni 6.8 wanashiriki katika Uchaguzi huu, nusu wakiwa ni vijana.