DRC-KIFO-ETTIENE

Mwili wa rais Ettiene Tshisekedi kurejeshwa nyumbani

Familia ya aliyekuwa kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Étienne Tshisekedi wa Mulumba, imesema mwili wa kiongozi huyo, utarejeshwa nyumbani tarehe 30 mwezi huu wa mei, na kuzikwa tarehe 01 juni.

Marehemu Etienne Tshisekedi,kiongozi wa zamani wa upinzani nchini DRC
Marehemu Etienne Tshisekedi,kiongozi wa zamani wa upinzani nchini DRC THIERRY CHARLIER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Imepita miaka miwili tangu Tshisekedi alipofariki dunia akiwa mjini Brussels nchini Ubelgiji mwezi Februari mwaka 2017.

Ni baba wa rais wa sasa Felix Tshisekedi.

Baada ya kifo chake kulizuka utata ni wapi atazikwa. Uongozi wa chama chake cha UDPS, ulitaka azikwe kwenye makao makuu ya chama hicho, katikati ya jiji kuu Kinsasha, lakini serikali wakati huo ikiongozwa na rais Joseph Kabila ikakataa.

Hadi kufariki kwake, alikuwa kiongozi wa muda mrefu wa upinzani, akiongoza chama cha UDPS laini aliwahi kuhudumu kama Waziri Mkuu wakati wa utawala wa rais wa zamani Mobutu Seseko mwaka 1991,1992-1993 na baadaye 1997.

Aliwahi kuwania urais mara kadhaa nchini humo hivi karibuni ikiwa dhido ya rais wa zamani Joseph Kabila.