MALAWI-SIASA-UCHAGUZI-WABUNGE-URAIS

Raia nchini Malawi wasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu

Raia wa Malawi wanasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu baada ya kupiga kura siku ya Jumanne, kumchagua rais na wabunge.

Mpiga kura nchini Malawi Mei 21 2019
Mpiga kura nchini Malawi Mei 21 2019 mbctv.malawi
Matangazo ya kibiashara

Kura zimekuwa zikihesabiwa usiku kucha huku ushindani wa ni nani atakayekuwa rais, ukisalia mkali.

Ushindani ni kati ya rais Peter Mutharika, aliyekuwa Makamu wa rais Saulos Chilima na Mhubiri wa zamani Lazarus Chakwera.

Tume ya Uchaguzi imesema kuwa zoezi lilikwenda vizuri na matkeo ya nwisho yanatariwa siku ya Jumatano au Alhamisi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jane Ansah amesema hakuna njia ya mkato kupata matokeo, wakati huu kura zikiendelea kuhesabiwa na amewataka raia wa nchi hiyo kuwa watulivu na kuepuka matokeo ya kupotosha.

Matokeo yameanza kuwasili katka kikao kikuu cha kujumuisha matokeo jijini Blantyre lakini hajawekwa wazi.