MALAW-MUTHARIKA-CHAKWERA-SIASA-MATOKEO

Ushindani mkali washuhudiwa Malawi kati ya rais Mutharika na Chakwera

Rasia wa Malawi ambaye pia ni kiongozi wa Chama tawala cha DPP, Profesa Peter Mutharika
Rasia wa Malawi ambaye pia ni kiongozi wa Chama tawala cha DPP, Profesa Peter Mutharika The Maravi Post

Matokeo ya urais nchini Malawi yanaonesha kuwa kuna ushindani mkali kati ya rais Peter Arthur Mutharika na mgombea wa upinzani Lazarus Chakwera.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, mgombea wa upinzani anaonekana kuwa mbele kwa karibu kura elfu 10, wakati huu kura zikiendelea kujumuishwa na maafisa wa Tume ya Uchaguzi.

Chakwera anaongoza kwa kura Laki 533, huku rais Mutharika akiwa na kuta Laki 524.

Mgombea wa upinzani Lazarus Chakwera anaonya uwezekano wa kutokea kwa wizi wa kura, wakati huu Tume ya Uchaguzi ikitarajiwa kutangaza matokeo ya mwisho baadaye hivi leo.

Chakwera amesema chama chake cha Malawi Congress Party (MCP) kinafanya mahesabu yake na kina uhakika wa kupata ushindi.

"Hadi sasa ujumbe upo wazi, tunajua kuwa tunaongoza," alisema mjini Blantyre.

"Hakuna anayekwenda kuiba uchaguzi huu.Haki itatendeka."

Waangalizi wa Uchaguzi wanasema zoezi hilo la upigaji kura zilifanyika kwa amani na utulivu.