CAR-MAUAJI-SILAHA-AMANI

Watu wenye silaha wawauwa watu 30 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Zaidi ya watu 30 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya kundi la washambuliaji waliojihami kwa silaha kuvamia vijiji vya Kaskazini Magharibi mwa Jamuhuri ya frika ya Kati .

Wapiganaji wa Seleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
Wapiganaji wa Seleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Umoja wa Mataifa linalolinda amani nchini humo MINUSCA limedai kuwa mauaji hayo yalifanyika katika vijiji kadhaa jirani na mji wa Paoua,mpakani mwa nchi ya Chad.

MINUSCA imesema wahalifu waliwasili vijijini na kuanza kufyatulia risasi wakaazi kiholela.

Jumla ya watu 31 waliuawa Koundjili na Lemouna huku takribani watatu wakiuawa Bohong.

Aidha, jeshi la polisi katika vijiji hivyo nalo limearifu vifo 15 katika kijiji cha Maikolo village, idadi ambayo umoja wa mataifa haikuithibitisha.

Haya yanakuwa mauaji makubwa kutekelezwa tangu serikali na wanamgambo kutiliana saini ya makubaliano ya amani mnamo mwezi wa pili yaliyolenga kurejesha maridhiano katika taifa hilo la Afrika ya Kati.