WHO-MALARIA-ALGERIA-ARGENTINA

WHO: Hakuna tena Malaria nchini Algeria na Argentina

Mbu anayesambaza Malaria
Mbu anayesambaza Malaria AFP/PHILIPPE HUGUEN

Algeria na Argentina zimethibitishwa na kutambulika rasmi na Shirika la afya ulimwengu WHO kuwa zimetokomeza ugonjwa wa malaria.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inamaanisha katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, hakujaripotiwa hata kisa kimoja cha mgonjwa wa malaria katika nchi hizo.

Malaria ugonjwa unatokana na kuumwa na mbu umesalia kuwa ni moja ya magonjwa yanayoongoza kwa vifo duniani.

Inakadiriwa kuwa mwaka 2017 pekee kulikuwa na visa Milioni 219 na vifo zaidi ya Laki Nne vya malaria, huku aslimia karibu 60 ya vifo hivyo vikiwa vya  watoto wa umri wa chini ya miaka 5.

Algeria ni nchi ya pili katika ukanda wa Afrika wa WHO kutambuliwa rasmi kama imetokomeza malaria baada ya Mauritius ambayo ilithibitishwa rasmi mwaka  1973.