DRC

DRC: Watu 30 wapoteza maisha katika ajali ya boti

Watu 30 wameripotiwa kupoteza maisha katika ajali ya boti na wengine mamia wakiwa hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama kwenye ziwa moja magharibi mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Rais wa DRC  Félix Tshisekedi
Rais wa DRC Félix Tshisekedi Félix Tshisekedi
Matangazo ya kibiashara

Meya wa mji wa Inongo, Simon Mbo Wemba amethibitisha kutokea kwa ajali hii ambapo amesema watu 30 wamekufa huku wengine zaidi ya 183 wakiokolewa.

Taarifa zinasema ajali hiyo ilitokea mwishoni mwa juma katika ziwa Mai-Ndombe ambapo boti hiyo ilikuwa imebeba watu zaidi ya 350 kwa mujibu wa mashuhuda.

Taarifa zaidi zinasema idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa kuwa zoezi la uokoaji bado linaendelea na kwamba hata hivyo hawajajua idadi hasa ya watu waliokuwa wakisafiri na boto hiyo.

Usafiri wa kwenye mito na maziwa ni miongoni mwa vyanzo vinavyotumiwa sana nchini DRC ambapo ajali za namna hii zimekuwa za kawaida kushuhudiwa kutokana na nyingi kubeba watu kuzidi uwezo.

Kumekuwa pia na idadi kubwa ya watu wanaopoteza maisha kwenye ajali hizo kutokana na wengi wa raia wa DRC hawafahamu kuogelea wala hazina maboya ya kujiokoa.

Mwezi uliopita watu 167 walipoteza maisha katika ajali mbili tofauti ambazo zilisababisha rais Felix Tshisekedi kuagiza kila boti lazima iwe na maboya ya watu kujiokoa.

Watu 27 waliripotiwa kupoteza maisna baada ya boti yao kuzama mwezi September mwaka jana, 26 wakipoteza maisha mwezi Julai mwaka jana, huku mwezi Mei mwaka huu watu 40 walipoteza maisha.