DRC-WAASI-ADF-USALAMA

Waasi wa ADF Nalu wawaua raia 12 mjini Beni

Kundi la waasi linaloaminiwa kuwa la ADF Nalu, wamewauwa raia 12 katika mji wa Beni, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wanajeshi wa DRC wakishika doria Mashariki mwa DRC
Wanajeshi wa DRC wakishika doria Mashariki mwa DRC Reuters
Matangazo ya kibiashara

Meya ya mji huo Modeste Bakwanamaha amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, ambayo amesema yamekuwa yakishuhudiwa tangu siku ya Jumatatu.

Ripoti zinasema kuwa waasi hao walitekeleza mashambulizi hayo  katika kambi ya jeshi la Rwangoma, lakini wakalemewa na kutoroka.

Mkuu wa Wilaya ya Rwangoma Richard Paluku, amesema pia wanajeshi wawili pia waliuawa katika makabiliano hayo.

Tangu mwaka 2014, makundi ya waasi wamekuwa wakishambuliwa katika makaazi yao, suala ambalo limewakasirisha wakaazi wa mji huo wakitaka serikali kufanya juhudi za kuimarisha usalama.