Pata taarifa kuu
SUDAN-JESHI-MAANDAMANO-BASHIR-SIASA-MAUAJI

Jeshi nchini Sudan lasema lipo tayari kwa mazungumzo

Wanajeshi walivyosambarataisha kambi ya waandamanaji jijini Khartoum nchini Sudan
Wanajeshi walivyosambarataisha kambi ya waandamanaji jijini Khartoum nchini Sudan ASHRAF SHAZLY / AFP
Ujumbe kutoka: Victor Melkizedeck Abuso
1 Dakika

Kiongozi wa kijeshi nchini Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan anasema jeshi liko tayari kwa mazungumzo baada ya machafuko yaliyotokea kuanzia siku ya Jumatatu na kusababisha vifo vya zadi ya watu jijini Khartoum.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, baadhi ya miili imepatikana ndani ya Mto Nile, wakati huu madaktari wakisema kuna idadi kubwa ya watu waliojeruhiwa na wanaoendelea kupewa matibabu baada ya kujeruhiwa.

Takwimu hizi zimetolewa na Madaktari nchini humo lakini pia makundi ya wanasiasa wa upinzani ambayo yamelaani mauaji hayo.

Ripoti zinasema kuwa, wanajeshi wanafanya ziara katika barabara za jiji la Khartoum, kuhakikisha kuwa hakuna waandamanaji wanaonekana, huku milio ya risasi ikisikika.

Machafuko yalizuka siku ya Jumatatu, baada ya jeshi kuamua kuvunja kambi ya wakimbizi waliokuwa wanaendelea kushinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.

Hatua hiyo imelaaniwa vikali na mataifa ya Magharibi lakini Urusi na China zimezuia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kulaani mauaji yaliyotokea nchini Sudan.

Baada ya hatua hiyo, jeshi liliamua kufuta makubaliano na viongozi wa waandamanaji kuhusu kuundwa kwa serikali ya mpito kwa kipindi cha miaka mitatu, na badala yake kutakuwa na Uchaguzi Mkuu baada ya miezi tisa.

Hata hivyo, viongozi wa waandamanaji wamekataa uamuzi huo wa wanajeshi na kusema wataendelea kuandamana.

 

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.