CAMEROON-UN-USALAMA-AMANI

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yaitaka Jumuiya ya Kimataifa kuingilia mvutano nchini Cameroon

Mashirika karibu tisa ya kutetea haki za binadamu duniani yametoa wito kwa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kuingilia kati na kuchukua hatua kukemea vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa raia wa eneo linalozungumza Kiingereza nchini Cameroon.

Waandamanaji nchini Cameroon wanaoishi katika nchi zinazozungumza lugha ya Kiingereza
Waandamanaji nchini Cameroon wanaoishi katika nchi zinazozungumza lugha ya Kiingereza REUTERS/via Reuters TV
Matangazo ya kibiashara

Wametoa wito huu kupitia barua walioandikia Baraza hilo tarehe 3 mwezi Juni ambapo mashirika haya yametaka Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati kinachotokea kwenye eneo hilo ili kunusuru kile walichosema kutekelezwa kwa mauaji ya kupangwa dhidi ya raia.

Siku ya Jumanne,  mkuu wa eneo la ukanda wa Mashariki ya kati wa Umoja wa Mataifa Francois Louceny Fall alilieleza barazala usalama kuhusu hali tete ya usalama na hofu ya kutokea machafuko kwenye eneo hilo.

Wito wa mashirika haya umekuja wakati huu vikosi vya Serikali ya Cameroon vikinyooshewa vidole kwa kutekeleza vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya raia wa eneo hilo ambalo wanataka lijitenge na Cameroon.

Jumuiya ya kimataifa imeendelea kukosolewa kwa kukaa kimya huku mamia ya raia wakilazimishwa kuhama nyumba zao na kuwa wakimbizi.

Raia kutoka mataifa hayo wanataka kujitenga na kuunda nchi yao wanayosema itaitwa Ambazonia.

Viongozi wa wa wanaharakati kutoka maeneo hayo,wamesema serikali ya rais Paul Biya haina nia ya dhati ya kuja katika meza ya mazungumzo.