Pata taarifa kuu
SOMALIA-UKAME-NJAA-FEDHA

Umoja wa Mataifa wahofia ukame nchini Somalia

Mtoto mwenye utapia mlo nchini Somalia
Mtoto mwenye utapia mlo nchini Somalia (File | AP)
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Umoja wa Mataifa unasema nchi ya Somalia inakabiliwa na baa la njaa kwa sababu ya hali ya ukame ambayo imekuwa ikishuhudiwa katika maeneo mengi ya nchi hiyo kwa muda mrefu sasa.

Matangazo ya kibiashara

Mark Lowcock anayehusika na masuala ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa anasema hali inayoshuhudiwa nchini Somalia ni mbaya ndani ya  kipindi cha miaka 35.

Lowcock anaomba wahisani kusaidia kupatikana kwa Dola Milioni 45 ili kusaidia kupatikana kwa maji safi ya kunywa, chakula na mahitaji mengine ili kuwasaidia zaidi ya watu Milioni mbili.

UN inasema watu wengine Milioni 3.2 wanatarajiwa kukabiliwa na baa la njaa katika siku zijazo iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa, kwa sababu hali inaendelea kuwa mbaya.

Mbali na msaada huo wa dharura, Umoja wa Mataifa unaomba Dola Bilioni 1.09 kusaidia kukabiliana na hali hiyo mwaka huu lakini ni asilimia 22 ya fedha hizo ndio iliyopatikana.

Tangu mwaka 1992, Somalia imekuwa ikishuhudia ukame kwa sababu ya kiwango kidogo cha mvua.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.