AFRIKA-AMNESTY INTERNATIONAL

Ripoti: Nchi nyingi za Afrika zinasheria kali dhidi ya ushoga

Mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani yanasema kuwa karibu nusu ya mataifa ya Afrika yaliyoko kusini mwa Jangwa la Sahara yamepitisha sheria kali dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja maarufu kama "Ushoga".

Wanharakati wa mapenzi ya jinsia moja nchini Kenya Mei 24 2019 wakiwa nje ya Mahakama jijini Nairobi
Wanharakati wa mapenzi ya jinsia moja nchini Kenya Mei 24 2019 wakiwa nje ya Mahakama jijini Nairobi www.reuters.com
Matangazo ya kibiashara

Licha ya uwepo wa sheria kali dhidi ya ushoga, nchi nyingi hata hivyo zimeanza kulegeza msimamo wao kuhusu watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Mashirika hayo yanasema nchi 28 kati ya 49 yanasheria zinaoharamisha mapenzi ya jinsia, amesema afisa anayehusika na masuala ya ushoga kutoka shirika la Amnesty International.

Baadhi ya adhabu ni pamoja na kunyongwa chini ya utawala wa sharia, kama vile nchini Mauritania, Sudan na kaskazini mwa Nigeria, licha ya kuwa hakuna taarifa hasa za watu wangapi walinyongwa.

Kusini mwa Somalia, wanaume mashoga wanaaminika kuwa wamekuwa wakipigwa risasi hadharani kwenye maeneo yanayokaliwa na wanamgambo wa Al-Shabaab.

Hata hivyo Amnesty International inasema nchi za Angola, Msumbiji na Seychelles zimeachana na sheria hizo katika miaka ya hivi karibuni.

Mwezi uliopita mahakama ya juu nchini Kenya ilikataa kubatilisha sheria inayofanya kuwa ni kosa la jinai kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Chad, Nigeria na Burundi zenyewe zimetunga sheria kali kuhusu ushoga.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema sheria nyingi zilizopo zilitenegezwa wakati wa ukoloni.