EBOLA-DRC-UGANDA

Wataalamu waonya kuhusu hatari ya kuenea kwa maambukizi zaidi ya Ebola

Mkurugenzi wa kituo cha kimataifa cha utafiti, amesema taarifa za uwepo wa maambukizi mapya ya virusi vya Ebola kwenye eneo la Afrika magharibi ni suala lonaloogopesha.

Wataalamu wa Afya wakipuliza dawa kuua virusi vinavyosababisha Ebola nchini DRC
Wataalamu wa Afya wakipuliza dawa kuua virusi vinavyosababisha Ebola nchini DRC REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Karibu watu elfu 1 na 400 wamekufa kutokana na virusi vya Ebola Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

Mkurugenzi wa shirika la Welcome Trust, Daktari Jeremy Farrar amesema mlipuko wa ugonjwa huu ni mbaya zaidi tangu ule wa mwaka 2013-16 na kwamba hauoneshi dalili ya kudhibitiwa.

Mtoto wa miaka 5 ameripotiwa kufa kutokana na virusi vya Ebola nchini Uganda, baada ya kuwa ametoka na familia yake nchini DRC mwanzoni mwa juma.

Serikali ya Uganda sasa inaripoti kuwa watu wengine 7 wamethibitishwa kuwa na maambukizi.

Daktari Farrar amesema kuenea kwa maambukizi mapya ni “janga” lakini ni suala lisiloshangaza, akionya kuhusu uwezekano wa kutopotiwa maambukizi zaidi.

Kwenye taarifa yake daktari Farrar amesema juhudi za haraka za jumuiya ya Kimataifa zinahitajika ili kuokoa maisha ya watu.

Tangu kuripotiwa kwa kisa cha mgonjwa wa kwanza mwezi Agost mwaka jana nchini DRC, watu elfu 1 na 400 wameshakufa huku karibu asilimia 70 ya watu wameambukizwa.

Mlipuko huu ni wa pili kwa ukubwa kuripotiwa katika historia ya ugonjwa wenyewe.

Ni mara moja peke yake imetokea kwa ugonjwa kuendelea kuenea ikiwa ni zaidi ya miezi 8 tangu uliporipotiwa na huu ulikuwa ni mlipuko wa Ebola kule Afrika Magharibi mwaka 2013 hadi 2016 ambapo Watu elfu 11 walikufa.