Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-UGAIDI

UNICEF: Watoto walitumiwa kutekeleza mashambulizi ya kigaidi nchini Nigeria

Wanajeshi wa Nigeria wakipiga kambi huko Maiduguri, Kaskazini mwa nchi hiyo
Wanajeshi wa Nigeria wakipiga kambi huko Maiduguri, Kaskazini mwa nchi hiyo REUTERS/Joe Brock
Ujumbe kutoka: Victor Melkizedeck Abuso
Dakika 2

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto UNICEF, linasema watoto walitumiwa kutekeleza mashambulizi ya kujitoa mhanga, yaliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kusababisha vifo vya wtau 30 na wengine 40 kujeruhiwa.

Matangazo ya kibiashara

Imebainika kuwa wasichana wawili na mvulana mmoja ndio waliotekeleza mashambulizi hayo katika ukumbi ambao ulikuwa umejaa watu waliokuwa wanatazama mchezo wa soka katika kijiji cha Konduga katika jimbo la Borno.

Hata hivyo, UNICEF haijaweza kubaini umri wa watoto hao.

Hii sio mara ya kwanza kwa kundi la Boko Haram kuwatumia watoto kutekeleza mashambulizi ya kigaidi, na imekuwa ikifanyika katika siku za hivi karibuni.

Ripoti ya Shirika hilo inaonesha kuwa watoto 48 walitumiwa kutekeleza mashambulizi ya kujitoa mhanga mwaka 2018, huku 38 wakiwa ni wasichana.

UNICEF inataka wale wote wanaowahusisha watoto katika suala hili la ugaidi, kuacha kufanya hivyo na badala yake kuwalinda.

Kundi la Boko Haram ambalo liliundwa mwaka 2002 limeendelea kuwa tishio kubwa kwa nchi ya Nigeria, hasa maeneo ya Kaskazini Mashariki na kuwa tishio la usalama wa nchi jirani za Afrika Magharibi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.