SUDAN-ETHIOPIA-SIASA-MAZUNGUMZO

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kuzuru tena Sudan

Waziri Mkuu wa Ethiiopia  Abiy Ahmed alipokutana na viongozi wa kijeshi
Waziri Mkuu wa Ethiiopia Abiy Ahmed alipokutana na viongozi wa kijeshi AFP

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anazuru tena jijini Khartoum nchini Ethiopia, kufuatilia mazungumzo kati ya uongozi wa kijeshi na viongozi wa waandamanaji.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa Abiy anakwenda na ujumbe wa kuomba pande zote mbili kukubadili mapendekezo ya kugawana madaraka kwa kipindi cha mpito.

Ripot zinasema kuwa makubaliano ya kugawana madaraka yamejadiliwa na kuandaliwa jijini Addis Ababa.

Tarehe 7 mwezi Juni, Abiy alizuru tena nchini Sudan na kukutana na pande zote mbili ambazo zilikubali kuja kwenye meza ya mazungumzo.

Mapendekezo yanayopendekezwa ni pamoja na serikali ya mpito kuundwa na wawakilishi nane kutoka upande wa kiraia na saba upande wa kijeshi.

Kiongozi wa kijeshi nchini humo Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, amekuwa akisema kuwa yuko tayari kwa mazungumzo ya viongozi wa waandamanaji.

Watu zadi ya 100, walipoteza maisha mapema mwezi huu baada ya jeshi kuamua kuvunja maandamano ya raia nje ya makao makuu ya jeshi.