Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-MACHAFUKO-USALAMA

Wahusika wakuu wa jaribio la mapinduzi waendelea kusakwa Ethiopia

Katika mtaa wa Lalibela, katika jimbo la Amhara, kaskazini mwa Ethiopia, Februari 2, 2019.
Katika mtaa wa Lalibela, katika jimbo la Amhara, kaskazini mwa Ethiopia, Februari 2, 2019. © REUTERS/Thomas Mukoya
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Vikosi vya usalama vya Ethiopia vinaendelea kuwasaka tangu jana Jumapili usiku wahusika wakuu wa mauaji ya wanasiasa nchini humo. Watu wanne waliuawa, ikiwa ni pamoja na Mkuu wa jeshi na rais wa Jimbo la Amhara, kaskazini-magharibi mwa nchi.

Matangazo ya kibiashara

Watu kadhaa wamekamatwa, lakini operesheni bado inaendelea, kulingana na msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu, baada ya kile serikali ya Ethiopia imesema kuwa lilikuwa "jaribio la mapinduzi".

Mamlaka inamshutumu mkuu wa usalama wa Amhara, Jenerali Asaminew Tsige, kuongoza jaribio hilo.

Jenerali Asaminew Tsige ambaye alikamatwa kwa njama ya madai ya kuhusika katika jaribio la mapinduzi la mwaka 2009, na kupewa msamaha wa rais mwaka 2018, amekimbilia mafichoni. Asaminew Tsige amekuwa akishikilia wadhifa muhimu katika mkoa huu unaokabiliwa na mgawanyiko mkubwa.

Katika taarifa yake, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema mkuu wa jeshi, Jenerali Seare Monnen, aliuawa nyumbani kwake kwa kupigwa risasi na mmoja wa walinzi wake, huku rais wa jimbo la Amhara, Ambachew Mekonnen akiuawa pamoja na mshauri wake.

Jenerali Seare aliuawa sambamba na Jenerali mwingine, Gezai Abera, na mlinzi ambaye sasa anashikiliwa, ofisi ya habari ya waziri mkuu imeeleza.

Mauaji haya yamezidisha shinikizo zaidi kwa waziri mkuu Ahmed ambaye ameendelea kutekeleza mabadiliko katika idara za usalama na kuwaachia wafungwa wa kisiasa.

Waziri mkuu alikwenda kwenye kituo cha Televisheni akiwa na mavazi ya kijeshi kukemea mashambulizi hayo.

Ofisi ya waziri mkuu imemshutumu mkuu wa usalama wa mji wa Amhara, Asaminew Tsige, kwa kupanga mapinduzi.Haijajulikana kama amekamatwa.

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yameikumba Amhara na miji mingine miaka ya hivi karibuni.

Tangu uchaguzi wa mwaka jana,Abiy amekua akipambana kumaliza mvutano wa kisiasa kwa kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, kuondoa makatazo dhidi ya vyama vya kisiasa na kuwashtaki maafisa wanaoshutumiwa kukiuka haki za binaadamu.

Ubalozi wa Marekani mjini Addis Ababa umewatahadharisha wafanyakazi wake mjini humo kutotoka nje, ikisema ina taarifa kuhusu mashambulizi ya risasi siku ya Jumamosi.Mtandao umekatwa tangu Jumamosi usiku.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.