Pata taarifa kuu
DRC-CENI-CENCO-SIASA

DRC: Kanisa Katoliki laomba CENI kufanyiwa mageuzi

CENI ilikosolewa mara kadhaa wakati wa mchakato wa uchaguzi ambapo Felix Tshisekedi aliibuka mshindi.
CENI ilikosolewa mara kadhaa wakati wa mchakato wa uchaguzi ambapo Felix Tshisekedi aliibuka mshindi. Caroline Thirion / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Muhula wa maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini DRC, CENI, unamalizika Juni 30. Na mazungumzo ya kuchukua nafasi za maafisa hao yanaendelea, kwa mujibu afisa mmoja wa mamlaka hiyo akinukuliwa na BBC Afrique.

Matangazo ya kibiashara

Siku chache kabla ya tarehe hiyo, Kanisa Katoliki limevunja ukimya wake na kuomba mamlaka hiyo ifanyiwe mageuzi.

"Marekebisho ya sheria ya uchaguzi kwa lengo la kutotumia kisiasa Tume Huru ya Uchaguzi, CEN,I ni muhimu," amesema Askofu Donatien Nshole, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (CENCO).

Kwa sheria ya sasa, CENI inapaswa kuongozwa na wajumbe kutoka vyama vya siasa na vyama vya kiraia.

Nafasi ya naibu mwenyekiti wa mamlaka ya uchaguzi inapewa na chama chenye viti vingi bungeni. Msemaji wa mamlaka hiyo hutoka katika kambi ya upinzani. Mwenyekiti anachaguliwa na dini mbalimbali.

CENI ilikosolewa mara kadhaa wakati wa mchakato wa uchaguzi ambapo Felix Tshisekedi aliibuka mshindi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.