Mauaji nchini Ethiopia yanalenga kuharibu mipango ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed ?

Sauti 12:47
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akiwa anatokwa na machozi wakati wa misa ya kumbukumbuka aliyekuwa mnadhimu wa jeshi Jenerali Seare Mekonnen Juni 25 2019
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akiwa anatokwa na machozi wakati wa misa ya kumbukumbuka aliyekuwa mnadhimu wa jeshi Jenerali Seare Mekonnen Juni 25 2019 AP

Mnadhimu Mkuu wa jeshi  nchini Ethiopia Jenerali Seare Mekonnen ameuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake jijini Addis Ababa, sawa na rais wa jimbo la Amharic Ambachew Mekonen ambaye alishambuliwa na watu wenye silaha. Ni mauaji yanayokuja wakati huu, Waziri Mkuu Abiy Ahmed akiendeleza mageuzi nchini mwake.  

Matangazo ya kibiashara

Hii inamaanisha nini ? Tunachambua na wachambuzi wa siasa za Kimataifa Haji Kaburu, Comrad Sambala wote wakiwa jijini Dar es salaam nchini Tanzania. Emmanuel Makundi, anashiriki pia, ni Mwanhabari wa RFI Kiswahili.